JUMLA ya wanachama wanne kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) Manispaa ya Singida, wamejitokeza kugombea nafasi ya
Mwenyekiti wa Jimbo hilo katika uchaguzi utakaofanyika Aprili 17, mwaka
huu.
Ofisa Habari wa chama hicho Jimbo la Manispaa ya Singida, Sylvester
Mirambo aliwataja waliochukua fomu na kutia nia ya kugombea kuwa ni
pamoja na Diwani wa Viti Maalumu Manispaa ya Singida, Josephine
Lemoyani.
Mirambo aliwataja wanachama wengine wanaowania nafasi hiyo kuwa ni
Juma Saidi Ng’wadi, Lumbael Mjengi na Yassin Kaali. Kwa mujibu wa Ofisa
Habari huyo, nafasi hiyo ipo wazi baada ya aliyekuwa Mwenyekiti, John
Kumalija kung’olewa madarakani na uongozi wa ngazi ya juu kutokana na
kile walichodai kutoridhishwa na utendaji wake wa kazi.
Wakati huo huo, Mirambo alisema kuwa kutakuwa na uchaguzi wa
kumchagua mwanachama atakayeziba pengo la nafasi ya Katibu Vijana wa
chama hicho (Bavicha) ambapo watu watatu, akiwemo yeye, wamejitokeza.
Wengine ni Michael Mtaza na Amosi Gwau.
Post A Comment: