ads

Leo Tarehe 23 Aprili, 2016  Rais Yower Museveni wa Uganda amemaliza sintofahamu iliyokuwa juu ya ni nchi gani kati ya Tnaxania na Kenya inastahili kujenga bomba la kusafirisha mafuta gafi kutoka Uganda.


Katika mkutano wa 13 wa Northern Corirodor uliohohudhuriwa na vongozi na wawakilishi wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki,akiwemo pia Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Paul Kagame wa Rwanda,Museveni amesema kuwa  wamekubaliana na Rais Uhuru Kenyatta kuacha mradi huo uendelee kama ulivyokubaliwa hapo awali ambapo ilikubaliwa kutumika kwa bandari ya Tanga badala ya ile ya Mombasa.


"Tumekubalina na Rais Uhuru Kenyatta juu ya kuuacha mradi huu uendele kama ulivyokuwa hapo awali,hivyo mchakato wa kufanikisha ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Ugnada hadi tnazania utaendelea kama kawaida"


Toka Rais Museven abadili maamuzi ya ujenzi wa bomba hilo kutoka bandari ya Mombasa nchini Kenya sakata hilo limekuwa likileta mkanganyiko kwa maofisa wa Serikali za Tanzania na Kenya 


Ambapo mara kadhaa Maofisa wa Serikali ya kenya wamekuwa wakizozana juu ya uhalali wa kujenga bomba hilo,Rais Museven alibadili uamuzi wa kujengwa kwa bomba hilo nchini Kenya mara baada ya kukutana na Rais Magufuli wa Tanzania wakati wa mkutano wa wakuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Arusha.

Katika kikao cha awali baina ya Rais Magufuli na Rais Museven,Rais Magufuli alimuhakikishia Rais Museveni kuwa Tanzania ni sehemu muafaka ya kujengwa kwa bomba hilo,huku kampuni ya Total ikitajwa kukubali kandarasi ya kujenga bomba hilo kutoka Uganda hadi Tanzania


DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA


ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: