Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimesema hakijaridhishwa na
uamuzi wa rais Dkt. John Magufuli kumsimamisha kazi aliyekuwa
Mkurugenzi wa Jiji, Wilson Kabwe huku aliyekuwa Meya Jiji Didas Masaburi
akiachwa.
Wakiongea
Jijini Dar es Salaam, Viongozi wa Chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam
akiwemo Makamu Mwenyekiti wa chama hicho ,Mkoa wa Dar es Salaam, Bernad
Mwakyembe na Katibu wake Henri Kileo , wamesema kuwa utumbuaji majibu wa
rais ni kama kiini macho kwa sababu hakuna mabadiliko yoyote kwa
wananchi wa Tanzania.
Aidha wametaka hatua stahiki zichukuliwe ikiwemo pamoja na kupelekwa mahakamani kwa wanaohusishwa na ubadhilifu huo ili hatua zaidi zichukuliwe ikiwemo na kurudishiwa fedha za wananchi walizozitafuta.
Aidha wameongeza kuwa Utenguzi wa Aliekuwa Mkurugenzi wa Jiji ungesubiri kikao cha baraza la madiwani ambacho kingefanyika na si vinginevyo na kuongeza kuwa rais angekuwa anawapa muda wa kujieleza wale wote wanaotumbuliwa.
Aidha viongozi hao wamesema kuwa rais anaonyesha kutumbua majipu lakini anaowatumbua sio wahusika wakuu wa ubadhirifu huo na kumtaka rais awatumbue na wale ambao wako nyuma ya pazia katika ufisadi huo.

DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: