Akizungumza na waandishi wa jijini Dar es Salaam jana, Kubenea alisema bajeti hiyo haikupitia katika baraza la madiwani la jiji kwa ajili ya kujadiliwa kama inavyotakiwa.
Alisema yeye akiwa mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tamisemi, amepanga kumuomba Spika airudishe bajeti hiyo ikajadiliwe na baraza hilo kwa ajili ya kujiridhisha kilichomo ndani yake ndipo irudishwe tena bungeni.
Kunenea alisema kama bajeti hiyo itawasilishwa bungeni atawashawishi wabunge wenzake kuikataa mpaka itakaporududishwa kujadiliwa na baraza la madiwani.
Alidai bajeti hiyo iliandaliwa na watendaji wa jiji na kupelekwa moja kwa moja Tamisemi, badala ya kupelekwa kwanza katika baraza hilo ili wajiridhishe kwa pamoja kiliochomo ndani yake.
“Bajeti za halmashauri zinapelekwa katika mabaraza ya madiwani, lakini cha kushangaza bajeti ya jiji haijapelekwa kwa madiwani wala mameya wa jiji husika ambao ndio wenye mkoa, watendaji wa jiji wameiandaa bajeti hiyo na kuipeleka moja kwa moja Tamisemi,” alisema Kubenea na kuongeza:
“Huwezi kuandaa bajeti na kuipeleka pasipo kuwashirikisha wenye jiji, sasa hivi jiji la Dar es Salaam linashikiliwa na Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), hivyo kufanya hivyo kunaweza kukawa ni njama za kuikwamisha ili waonekane wameshindwa na kusababisha kuvunjwa baraza la madiwani, hatukubali njama hizi tunazifahamu.”
Kubenea alisema njama za namna hiyo wanazifahamu na kwamba hawawezi kuruhusu ziendelee kufanyika isipokuwa watapambana hadi kuhakikisha kila kitu kinawekwa wazi.
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: