Mwanamuziki gwiji wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Papa
Wemba (pichani), amekufa baada ya kuanguka stejini wakati akitumbuiza
mjini hapa, imeelezwa.
Picha ya video ya onesho hilo ilionesha wasanii
wake wakiendelea kucheza wakati mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 66
akiwa ameanguka chini jukwaani huku wasanii wake wasijue kilichotokea.
Televisheni ya Ufaransa ya France 24 ilithibitisha kifo hicho cha
Papa Wemba, wakimnukuu meneja wake. Mwanamuziki huyo alikuwa katika
medani ya muziki wa Afrika tangu mwaka 1969, ambapo alitwaa tuzo ya
dunia kufuatia mtindo wake wa “Rumba Rock”.
Mwaka 2004, mwanamuziki huyo alipatikana na hatia nchini Ufaransa ya
kuingiza wahamiaji haramu, ambapo alifungwa jela miezi mitatu. Mwamuziki
huyo bado ataendelea kuwa mmoja wa wanamuziki hodari wa Afrika.
Soukous, ambayo pia inajulikana kama Rumba Rock, ilikuwa maarufu
Afrika nzima. Pamoja na bendi zake za Zaiko Langa Langa, Isifi na ile ya
Viva La Musica, aliibuka na vibao vikali kikiwemo kile cha L’Esclave na
Le Voyageur.
Pia mwamuziki huyo aliwahi kufungwa jela nchini mwao Kongo. Shitaka
lake nchini Ufaransa lilihusiana na kupanga njama, ambapo alikuwa
akisaidia wahamiaji kuingia Ulaya akidai ni wanamuziki wa bendi yake.
Rapa wa jijini Kinshasa Youssoupha aliomboleza katika twitta (nchini
Ufaransa), akisema, “Kama jamii, amesikitishwa na kifo cha Papa Wemba.”
“Alikuwa mfano katika utamaduni wetu, hivyo ni pigo kubwa katika jamii
yetu.”
DOWNLOAD
APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA
KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD
BONYEZA HAPA
Post A Comment: