ads

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi Hamad Masauni amewasimamisha kazi watumishi wa tatu wa jeshi la Polisi kikosi cha zimamoto wa Uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa kosa la kuiba mafuta ya ndege na kuiba mizigo ya abiria hali inayohatarisha usalama wa abiria na mali zao.


Akiwataja waliosimamishwa kazi ni pamoja na Halfani Kisana na Mussa Mandauli ambao walitumia gari la Mkuu wa kikosi cha zima moto kuiba mafuta ya ndege lita 200 na Abias Mwanza ambae alishirikiana na Lucas Maganda mtumishi wa swissport kwenye wizi wa mizigo ya abiria ambayo ilikuwa imehifadhiwa eneo la kihifadhi mizigo.

Askari hao baada ya kufanya uhalifu huo baadhi yao walipandishwa vyeo na wengine kuhamishiwa Makao Makuu ya Jeshi la Zimamoto bila ya kuchukuliwa hatua zozote za kinidhamu na kisheria.

Aidha naibu waziri amelitaka jeshi la polisi kufuatilia waliokuwa wanaendesha magari mawili yenye namba za usajili T225 AWN Saloon GX210 na T786AWZ kwani magari hayo yanatumika kusafirishia mafuta toka uwanja wa ndege hivyo wanatakiwa waeleze ni nani anawatuma na wanayapeleka wapi, endapo watakutwa na hatia zozote wachukuliwe hatua .

Kwa upande wake Mkuu wa Polisi wa Viwanja vya ndege Martin Otieno amesema kuwa kikosi chake kinakabiliwa na upungufu mkubwa wa rasilimali watu na vitendea kazi hali inayowapelekea kufanya kazi kwenye mazingira magumu.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: