Asali
ni tiba karibu kwa kila ugonjwa. Matumizi ya asali kama tiba kwa
magonjwa mbalimbali ni kitu ambacho kinafahamika kwa karne nyingi
zilizopita duniani kote. Vitabu
vingi vya zamani vimeandika namna watu walivyotibiwa magonjwa
mbalimbali kutokana na asali.
Sasa hivi kuna makala nyingi zilizo
andikwa zikielezea kuhusu uwezo wa asali katika tiba ya magonjwa
mbalimbali.Warusi na Wafaransa wanafahamika sana katika kufanya utafiti
katika maabara kuhusu uwezo wa asali katika tiba mbalimbali.
Katika makala hii tutaangalia tiba ya asali na mdalasini
na namna ya kuitumia kutibu maradhi mbalimbali (asali tunayoizungumzia
hapa ni asali safi yaani asali mbichi ya nyuki wakubwa na wadogo).
YAFUATAYO NI BAADHI YA MARADHI YANAYOTIBIKA KWA ASALI NA MDALASINI:
1. Ugonjwa wa viungo, maumivu na uvimbe
-Chukua maji kiasi vuguvugu na ongeza mdalasini, unga kijiko cha chai na asali vijiko 2 vya chakula na kuchua sehemu zenye maumivu.
-Vilevile waweza kutengeneza kikombe kimoja cha chai kwa kuweka
kijiko kimoja cha unga wa mdalasini na kuongeza asali vijiko viwili vya
chakula na kisha kunywa ikiwa ya moto kutwa mara mbili.
2. Kukatika kwa nywele
-Asali ikichanganywa na mdalasini na mafuta vuguvugu ya mzeituni hutia kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele.
-Tumia mchanganyiko huo vuguvugu kwa kupaka na kusugua kichwani na acha kwa dakika 15 kisha uoshe.
-Tumia mchanganyiko huo vuguvugu kwa kupaka na kusugua kichwani na acha kwa dakika 15 kisha uoshe.
3. Ukungu wa miguu au fungus
-Changanya kijiko cha chakula cha asali na vijiko viwili vya chai vya
mdalasini na acha kwa muda wa nusu saa kisha safisha (rudia hivyo mpaka
upone).
4. Maambukizi kwenye kibofu cha mkojo
-Changanya maji ya uvuguvugu na vijiko 2 vya chai vya mdalasini na kijiko1 cha asali huondoa bakteria kwenye kibofu.
5. Maumivu ya jino
-Chukuwa mdalasini ya unga kijiko kidogo kimoja, changanya na asali
vijiko vitano kisha dondoshea kwenye jino linalouma kutwa mara mbili
hadi maumivu yatakapotoweka.
6. Vidonda vitokanavyo na magonjwa ya kulala kwa muda mrefu
-Paka saladi iliyochanganywa asali na mdalasini.Vilevile tumia chai ya roseberry nyekundu kwa kuondoa aina hii ya maumivu.
7. Lehemu
-Changanya asali safi mbichi vijiko 2 vya chakula na unga wa
mdalasini vijiko 2 vya chakula na kikombe cha chai cha maji ya moto na
unywe kutwa mara 3
8. Mafua
-Tumia mchanganyiko wa kijiko 1 cha chakula cha asali vuguvgugu na
robo kijiko cha unga wa mdalasini kuondoa chafya na kuvimba koo.
9. Ugumba
-Asali inaaminika kuamsha hamu ya mapenzi. Wapenzi wa jinsia zote
wanashauriwa kunywa walau vijiko 2 vya chakula kila siku kabla ya muda
wa kulala. Mdalasini imetumika muda mrefu katika dawa za kichina na
kihindi kuongeza uwezo wa uzazi kwa akina mama wenye kuhitaji kuzaa
-Changanya mdalasini na kiasi cha asali na kufanya mgando (paste) na
upake kwenye fizi na meno na kuacha inyonywe na kuingia mwilini taratibu
na hii ni kwa akina mama wasio na sababu za kimsingi za kuwakosesha
kuzaa.
10. Mchafuko wa tumbo
-Asali kwa muda mrefu imetambulika kama dawa ifaayo kuondoa mchafuko
wa tumbo na kichefuchefu. Ongeza kiasi kidogo cha mdalasini na asali pia
hupunguza maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.
11. Gesi au Asidi
-Kula asali pamoja na mdalasini kuondoa mchafuko wa tumbo uletwao na
gesi (acid) na huu ni uchunguzi ulio fanywa na Japan na India
12. Ugonjwa wa moyo
-Unaweza kujikinga kupata ugonjwa wa moyo na kuzuia mkusanyiko wa
mtandao wa mafuta kwenye mishipa ya damu kwa kula asali na mdalasini
mara kwa mara kwa kupakaa kama jam wakati wa kula mkate wa ngano wenye
nyuzinyuzi nyingi iliyopakwa kijiko 1 cha chakula cha mchanganyiko huo
(asali na mdalasini) kila siku.
13. Shinikizo la juu la damu
-Shinikizo la damu
pamoja na matatizo yaambatanayo na maumivu ya kifua na kizunguzungu
yalitoweka kutoka kwa wagonjwa wengi wiki chache tu baada ya kupata dozi
ya mara kwa mara ya asali iliyochanganywa na mdalasini.
14. Kinga ya mwili
-Kinga yako ya mwili itaongezeka mara tatu zaidi ikiwa utatumia mara
kwa mara asali na mdalasini kwa pamoja. Utafiti unaonyesha kuwa hazina
kubwa ya vitamini (virutubisho), madini pamoja na mchanganyiko wa
mdalasini na asali iondoayo magonjwa na kinga itolewayo na chembechembe
nyeupe za damu husaidia kuzuia magonjwa pamoja na kuharibu vimelea na
bakteria.
15. Ukosefu wa nguvu za kiume
-Asali ina historia ndefu ya kuamsha nguvu ya uume pamoja na kuwa
dawa madhubuti ya kuponyesha uhanithi kutokana na uwezo wake kama
kiamshaji/chaji. Asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya
dini za mashariki za dunia. Watafiti wa kiaustralia waligundua kwamba
asali inauwezo wa kupelekea mwili kutoa homoni mbalimbali kama ilivyo
mdalasini.
-Katika Afrika na dunia ya kusini mabaharia wamekuwa wakipaka asali
katika sehemu zao za nje ya uume ili kuongeza nguvu ya kufanya mapenzi.
Post A Comment: