Rais Barack Obama wa Marekani
amelaumu vyombo vya habari kwa kukua kwa umaarufu wa mgombea wa tikiti
ya chama cha Republican Donald Trump.
Akihudubia hafla maalum kwaajili ya waandishi wa habari wa siasa bw
Obama alisema sharti waandishi wa habari nao wawajibike kwani haitoshi
tu ”kumpa mtu kinasa sauti ”
Bwenyenye huyo mbishi ambaye alijenga jina lake na kupata utajiri
mkubwa kutokana na kuendesha na kumiliki migahawa katika maeneo mengi tu
duniani anapigiwa upatu kutwaa tikiti ya chama cha Republican kuwania
urais.
Trump, na wapinzani wake wanaowania tikiti ya chama chao cha
Republicans wameratibiwa kukabiliana katika mdahalo wa runinga baadaye
leo usiku.
Shirika la habari la CNN linaanda madahalo huo kabla ya kura za
mchujo za jimbo la Wisconsin zinazoratibiwa kufanyika juma lijalo.
Japo hakumtaja Trump kwa jina ilikuwa bayana kuwa ndiye aliyelengwa na ujumbe wa Obama.
Anaposafiri ughaibuni, Obama anasema watu humuuliza nini
kinachoendelea katika siasa za Marekani kwani’ sio mahali unakotarajia
siasa zisizokuwa za kawaida”
Wanasiasa waandishi habari na umma kwa jumla wana wajibu wakati wa siasa kali kama hizi zinazoshuhudiwa kwa sasa Marekani.
Aliwashauri waandishi habari kupiga msasa habari wanazochapisha.
Haiwezekani kuwa mwanasiasa anaahidi vitu ambavyo tunajua wazi kuwa
hawezi kutimiza ilahali anaendelea kupeperushwa hewqani ,lazima nanyi
mchukue jukumu la kuuliza maswali magumu na kutofautisha mbivu na
mbichi.
Katika siku za hivi punde Trump alikashifiwa na wapinzani wake kwa
kumgoa mkewe mpinzani wake ambaye ni gavana wa jimbo la Texas Ted Cruz.
Trump atakabiliana na mpinzani wake mkuu Ted Cruz katika uchaguzi wa jimbo la Wisconsin Aprili tarehe 5.
Post A Comment: