Kuwa na harufu mbaya mdomoni ni kitendo kinachoweza kuathiri maisha
ya mtu kimahusiano si kwa mpenzi tu bali marafiki na jamii kwa ujumla.
Pia kuwa na harufu mbaya mdomoni uondoa haiba ya kupendwa kwani hata
unapoongea wengi watakwepa kuongea moja kwa moja na wewe kwa sababu ya
harufu mbaya inayotoka mdomoni mwako.
Chakula unachokula kina athiri hewa inayotoka mdomoni au sehemu nyingine
za mwili wako. Baadhi ya vyakula vina matokeo mabaya sana kwa hurufu
unayotoa mdomoni. Harufu mbaya mdomoni si ugonjwa wa kuambukiza haina
haja kuogopa ukikutana na mtu mwenye harufu mbaya mdomoni kwamba
atakuambukiza.
Pia tatizo kubwa ni kwamba watu wenye harufu mbaya mdomoni hawajijui
kwamba wana harufu mbaya. Asilimia 85 - 90% ya tatizo la harufu mbaya
mdomoni asili yake ni kinywa chenyewe. Pia kiwango cha harufu
hutofautiana kutokana na muda (mchana, usiku na asubuhi).
Harufu nyingi mbaya mdomoni hutokana na vyakula vyenye asilia ya
protein. Kuna zaidi ya aina 600 ya bacteria wanaoishi kwenye kinywa cha
Binadamu (sehemu ya juu ya ulimi, fizi na kuzunguka meno).
KINACHO SABABISHA HARUFU MBAYA MDOMONI
Kutokuwa makini na usafi wa kinywa kama vile kupiga mswaki vizuri
kunakoacha mabaki ya chakula ambayo huoza na kusababisha harufu mbaya
mdomoni. (Wengi hupiga mswaki haraka haraka na kuacha mabaki ya
chakula). Maambukizi ya magonjwa kama vile fizi kutoka damu, mfumo wa
upumuaji na kisukari. Kinywa kuwa kikavu kutokana na madawa
(medications) Kuvuta sigara, kunywa kahawa, ulaji wa vyakula vyenye
viungo vikali kama vile vitunguu maji au thaumu.
NAMNA YA KUJUA KAMA UNA HARUFU MBAYA MDOMONI
Wanasayansi wamekiri kwamba ni ngumu sana mtu kujijua mwenyewe kama ana harufu mbaya kwa sababu ya mazoea (habituation).
Ni rahisi sana kutambua harufu kutoka kwenye kinywa cha mtu mwingine.
Unaweza kutambua kama una harufu mbaya mdomoni kwa kumuuliza mtu
unayemuamini.
Pia unaweza kujua harufu mbaya kwa kulamba nyuma ya kiganja na kunusa,
wengine hupumua mbele ya kioo na kunusa. Pia unaweza kutumia kijiti cha
kuchokonolea meno na kukinusa. Kisayansi unaweza kutumia vifaa kama
Halimeter, Gas Chromatography na BANA Test.
NAMNA YA KUJILINDA NA HARUFU MBAYA MDOMONI (TIBA)
Kula vyakula vyenye afya na vyakula ambavyo wakati unakula vinaweza
kusafisha kinywa vizuri. Kusafisha meno mara kwa mara au kwa uchache
mara mbili kwa siku asubuhi na baada ya mlo wa usiku, hii usaidia
kuondoa au kujikinga na harufu mbaya mdomoni. Vilevile unashauriwa
kutumia KISAFISHA ULIMI (tongue cleaner) kusafishia ulimi wako.
Tumia
bazooka (chewing gum) ambazo husaidia kuongeza kiasi cha mate kwenye
kimywa kilichokauka. Baadhi ya gums zina viungo vinavyoondoa harufu
mbaya mdomoni na zingine husafisha kinywa na bacteria wanaosababisha
harufu mbaya. Tumia dawa ya kusukutua mdomoni (mouthwash) kabla ya
kulala usiku.
Kuwa makini na afya ya kichwa chako kama vile kupiga
mswaki vizuri, kuondoa mabaki ya vyakula kwenye meno na kumuona daktari
kila unapoona una Matatizo ya meno au kinywa au kila baada ya miezi sita
kwa uchache.
Kuhakikisha unakunywa maji ya kutosha kila siku angalau glass mbili za maji.
Mwone daktari wako ukiona una tatizo la harufu mbaya mdomoni.
NAMNA YA KUJIKINGA NA KUONDOA HARUFU MBAYA MDOMONI!
Watu wengi husumbuliwa na tatizo la kunuka mdomo bila hata kujijua hivyo
kuwa kero kwa wenzao na wakati mwingine hujishushia hadhi mbele ya
jamii. Mara nyingi ugonjwa wa kunuka mdomo (Halitosis) husababishwa na
uchafu wa kinywa na ulaji wa vyakula usiosahihi lakini ni tatizo
linalotibika.
Ni rahisi kulizuia na kuliondoa tatizo la kunuka mdomo iwapo utaamua
kufuata kanuni za usafi wa kinywa na unywaji wa maji kwa kufuata kwa
makini muongozo ufuatao:
KUPIGA MSWAKI
Kitu cha kwanza kufanya ni kupiga mswaki kwa ukamilifu kila uamkapo
asubuhi. Wakati wa kupiga mswaki, utatakiwa siyo tu kusugua meno, bali
pia ulimi, sehemu ya katikati hadi karibu na koromeo kwa kusugua
vizuri.
Vile vile kila uamkapo baada ya kulala mchana au jioni, hakikisha
unapiga mswaki, kwani bakteria wa kinywani, hutawala kinywa kila
ulalapo. Mara baada ya kupiga mswaki na kusugua ulimi sawaswa, hakikisha
unasukutua vizuri kwa maji, kwani hapa ndipo baadhi ya watu hukosea kwa
kupiga mswaki bila kusukutua kwa maji.
KUNYWA MAJI MENGI
Maji ni muhimu sana karibu kila eneo la mwili wa binadamu. Unywaji wa
maji ya kutosha kila siku utakusaidia kudhibiti na hatimaye kuondoa
tatizo la kunuka mdomo. Unywaji wa maji mengi ni muhimu, hasa kwa wale
watu wenye ugonjwa wa kukauka midomo (xerostomia).
Mara nyingi harufu itokayo mdomoni, hutokea tumboni na siyo kinywaji
peke yake kama unavyoweza kudhani. Hivyo, kama tumbo litakuwa chafu,
hata kama utasafisha kinywa vizuri bado harufu mbaya inaweza kuendelea
kutoka. Harufu mbaya ya tumboni hutokea pale tumbo linapokuwa chafu
kutokana na kutopata choo kwa muda mrefu.
Miongoni mwa mambo
yanayochangia kukosekana kwa choo kwa muda mrefu ni pamoja na tabia ya
kutokunywa maji ya kutosha kwa siku, hivyo hakikisha unakunywa maji,
kiasi kisichopungua lita moja na nusu hadi mbili au zaidi, kutegemeana
na kazi unazozifanya.
Ukiwa na tatizo la kukaukiwa maji mwilini kila mara, mwili hujaribu
kutumia njia zake za kiasili kupunguza uzalishaji wa mate ili kuhifadhi
maji kwa ajiili ya matumizi mengine, kitendo hicho huchangia kunukisha
mdomo kwa sababu ndani ya mate huwa kuna kinga muhimu dhidi ya baktetria
wanaonukisha kinywa.
Kwa upande mwingine, ili kuzuia kinywa kunuka pale mdomo unapokuwa
umekaukiwa na mate, ni vizuri kutafuna vitu kama bazooka (chewing gum)
yoyote ili kuzalisha mate ambayo huhitajika katika kudhibiti bakteria.
MWISHO:
Hakikisha
unasukutua sawaswa baada ya kula chakula chochote, hata kama ni juisi
isipokuwa unapokunywa maji tu ya kawaida. Bila shaka, ukizingatia haya,
tatizo ulilonalo la kunuka mdomo litataoweka na kubaki historia.
Post A Comment: