ads

Msanii mkongwe katika muziki wa bongo fleva KR Mullah ambaye kwa sasa amejiunga na Label ya 'Radar Entertainment' ambayo inaongozwa na msanii T.I.D amefunguka na kusema kuwa ikitokea mtu akamnyoa ndevu zake anaweza kufa hapo hapo kama Samsoni alivyonyolewa nywele na kuishiwa nguvu.

KR Mullar alisema haya alipokuwa kwenye kipindi cha eNEWS (EATV) na kudai kuwa hawezi kubadili muonekano wake huo japo anatambua kuwa unawatisha baadhi ya watu na wengine wanachukulia kama yeye ni mkorofi kutokana na muonekano wake huo.

"Ni kweli kuna baadhi ya watu huwa wananiogopa kutokana na muonekano wangu lakini mimi napenda sana watu nacheka sana na kila mtu na kikubwa napenda sana watoto, ingawa wakiniona hivi nilivyo watu wengine wanadhani kama nitawapiga hivi kumbe hakuna hilo.


ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: