ads

Walikuwa katika njia ya mafanikio, hatimaye muziki aliofanya 20% kwa miaka mingi ulianza kumpa matunda akiwa mikononi mwa  Man Water, mtayarishaji (Producer) mkubwa Bongo ambaye umahiri wake wa midundo ulipelekea 20% kuvunja rekodi ya kuchukua tuzo 5 mfululizo za KTMA.

Ghafla mambo yakaanza kwenda ndivyo sivyo na taarifa zikasambaa kuwa wawili hao hawafanyi tena kazi pamoja.

20% kafunguka kupitia Planet Bongo ya East Africa Radio na kueleza kuwa hata yeye hajui hasa nini kisa na mkasa cha kutengana kwao ila anahisi kuna watu walisababisha mtafaruku baina yao na amejaribu kumtafuta Man Water mara kadhaa kujua hasa nini kiini cha tatizo.

Siku za nyuma wawili hao waliwahi kutangaza kumaliza bifu lao na wangeendelea kufanya kazi pamoja jambo ambalo halikutokea na 20% aliwahi kunukuliwa akiwalaumu Madj wa Redio moja hapa bongo kuwa chanzo cha yote hayo.

Tangu 20% aondoke kwa Man Water ameshuka ksanaa na hasikiki tena licha ya kutoa ngoma kadhaa lakini hazijaweza kumuweka kwenye nafasi nzuri kama ilivyo tarajiwa na wengi.

Hata hivyo amesema bado hajachoka kumtafuta Man Water ili wayamalize na muda si mrefu huenda tukasikia yameisha.

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: