Mbunge wa Jimbo la Mikumi Mkoani Morogoro Joseph Haule amefanikiwa kupunguza tatizo la maji kwa wakazi wa jimbo hilo kwa kuchimba Kisima kikubwa kitakachowawezesha wakazi wa Mikumi kupata maji yaliyo safi na salama.
Mh Haule amesema kuwa amelazimika kuchimba kisima hicho ili kupunguza tatizo la maji wakati wakiendeleaa kutathmini namna nzuri zaidi ya kusambaza mabomba na kumaliza kabisa tatizo la maji katika mji mdogo wa Mikumi.
Jimbo la Mikumi hususan eneo la mji mdogo wa Mikumi kumekuwa na tatizo la maji kwa takribani miaka kumi sasa hali inayopelekea wanachi kununua maji lita ishirini kwa shilingi mia tano huku wengine wakilazimia wakazi wa mji huo kutembea umbali mrefu kutafuta maji.
Post A Comment: