Zoezi la kubomoa jengo lenye ghorofa 16 lililopo katikati ya jiji la
Dar es salaam limekamilika kabla ya muda ambapo jumla ya siku 46
zimetumika kukamilisha zoezi hilo badala ya siku 90 zilizotakiwa
kubomolea jengo hilo.
Akizunguza kwenye eneo la ubomoaji mkurugenzi wa manispaa wa Ilala
Isaya Mgulumi amesema zoezi hilo limetekelezwa na mkandarasi mzalendo
kwa gharama ya bilioni 1na limekamilika bila madhara yoyote hali ambayo
inaonyesha wakandarasi wa ndani wana uwezo mkubwa wa kiutendaji
wanachotaki ni kusimamiwa kwa karibu.
Jengo hilo pacha lililopo mtaa wa Indira Ghandi limevunjwa kufuatia
kuanguka kwa jengo lingine liliokuwapo mita chache kutoka katika jengo
hilo ambalo nalo lilijengwa ghorofa 16 badala ya ghorofa nane. Jengo
hilo liliporomoka na kusababisha vifo vya watu 34 july 23 mwaka 2013.
Pamoja na kuvunjwa kwa jengo hilo wamiliki wa jengo hilo, Mkandarasi,
Mkaguzi wa majengo pamoja na maafisa wa ardhi na manispaa
walioidhinisha ujenzi huo walifikishwa mahakamani huku mmiliki wa jengo
hilo akitakiwa kulipa gharama zote za ubomoaji wa jengo hilo.
Post A Comment: