ads

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela amesema mkoa wake hauna mfanyakazi hewa hata mmoja wakati wa uhakiki wa wafanyakazi uliofanyika mkoani humo.


Mama Kilango ameyasema hayo alipokuwa akiwasilisha serikalini ripoti ya mkoa wake kufuatia agizo la Rais kwa wakuuu wa mikoa kote nchini kuwasilisha majina ya watumishi hewa wanaoliingizia taifa hasara huku wakiwa hawapo kazini.

''Mkoa wa Shinyanga hauna mfanyakazi hewa hata mmoja kutokana na mpango waliojiwekea viongozi wa mkoa kwa kufuatilia watumishi waliopo kazini na kulipa mishahara kwa watumishi waliopo maeneo ya kazi pekee.'' Amesema Kilango.

Aidha kwa ripoti za wakuu wa mikoa zilizowasilishwa mkoa wa Mwanza unaongoza kwa kuwa na watumishi hewa 334 na Arusha 270 na Singida 231ikifuatiwa na mikoa mingine.

Hata hivyo waziri George Simbachawene amewataka wakuu wa Mikoa kuhakikisha wanaendeleza zoezi hilo kwani kuna wafanyakazi ambao wameaga wapo likizo na wengine masomoni wakati uhalisia haupo.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: