Staa wa muziki tanzania Rehema Chalamila amefungua mlango kwa mwanamume yeyote anayetaka kumuoa ilimradi awe na vigezo hivi 10 alivyoviainisha
kupitia ukurasa wake wa instagram Ray C ameandika haya
Habari zenu wapendwa dunia nzima leo nina habari nzuri kwenu , Naomba kuwatangazia kuwa natafuta mchumba wa kuishi nae milele na nimzalie watoto wawili wa kike na wakiume
ila naomba niwambie masharti kabisa
1. Awe mpole ili nikikasirika anibembeleze
2. awe anapenda muvi za kihindi ili nikiwa na stress aniwekee nyimbo za kihindi maana ndio raha ya moyo wangu
3. Asiwe muongeaji sana maana sipendi kelele
4. Anipende na ubonge wangu huu huu asije akaniambia baby anza mazozi au dah baby zamani ulikuwa bomba au rudisha kiuno hapo hatutoelewana
5. Awe ananipikia ninachotaka maana navutiwa sana nikimuona mwanaume akipika
6. Awe mvumilivu maana nikiwa na hasira huwa naongea kwa sauti ya juu sana
7. Asiwe na marafiki wengi, na akitaka kukutana nae nami niwepo maana si mnajua wanaume wakikutana huwa wanashauriana mabaya
8. Awe nami wakati wote maana nina wivu sana ikiwezekana tufanye kazi ofisi moja au awe ofisi ijengwe nyumbani
9. Awe anajua nyimbo zangu zote ndio nitaamini kuwa kweli ananipenda
10. Sharti la mwisho ni hili ambalo ni muhimu sana kwangu tuwe tunatumia simu moja na namba moja, maana hata kanisani tunafundishwa kuwa ndoa maana yake tumeungana na kuwa kitu kimoja kwa hiyo kama mume na mke tunalala kitanda kimoja na kuishi pamoja kwanini tusitumie simu moja! sioni tatizo.
Post A Comment: