Washambuliaji wa Yanga, Emmanuel Martin na Godfrey Mwashiuya,wamekuwa wakilalamikiwa na  mashabiki wao, kutokana na kukosa mabao ya wazi baada ya kocha kuwatumia badala Amissi Tambwe na Donald Ngoma ambao ni majerahi.


Mwashiuya na Martin, walikosa nafasi za wazi baada ya Yanga, kucheza  na watani wao wa jadi Simba, mchezo uliyomalizika kwa sare ya bao 1-1, Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

"Bado ligi inaendelea naamini nitafunga mashabiki wangu watanielewa kwa sasa ni ngumu kujua ni changamoto inayoweza kumpata mchezaji yoyote katika mpira wa miguu,"alisema.

"Kwanza makipa wa Yanga ni bora zaidi ila ukizungumzia upinzani basi Manula kwa kipindi hiki yupo vizuri, anastahili sifa hiyo,"aliongeza mchezaji huyo.

Lakini katibu wa zamani wa timu hiyo, Lawrence Mwalusako aliwataka Mwashiuya, Martin pamoja na Juma Mahadhi, kuonyesha uwezo kutokana na umri wao.

"Unaposema vijana maana yake damu zao zinachemka, waongezee bidii, wasichukulie kawaida nafasi wanayopewa na kocha, wajue usajili upo,hivyo uwezo wao ndiyo utakuwa kinga ya kubaki kwenye timu,"alisema.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: