ads

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetolea ufafanuzi wa sukari tani 6757 mali ya El-Naeem Enterprises iliyokamatwa hivi karibuni  katika bohari ya forodha ambapo imesema kuwa ilikuwa chini ya uangalizi ikisubiri vibali husika ili iweze kuruhusiwa kusambazwa nchini.


Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipakodi kutoka mamlaka ya mapato Tanzania, Richard Kayombo, amesema sukari hiyo ilikuwa katika bohari ya forodha ya uangalizi ya mamlaka ya mapato Tanzania ikiwa imehifadhiwa kusubiri kukamilishwa kwa utaratibu wa kodi, vibali vya mamlaka ya chakula na dawa TFDA na vibali vya bodi ya sukari na hatimaye kuweza kuruhusiwa kutoka.

Sukari hiyo kwa sasa imeruhusiwa kutolewa ambapo Channel Ten imefika katika bohari hiyo ya forodha na kushuhudia ikipakuliwa tayari kusambazwa nchini
 
DOWNLOAD APP YETU YA SWAHIBA NEWS ILI UWEZE KUPATA HABARI ZOTE MOJA KWA MOJA KUPITIA SIMU YAKO YA MKONONI BILA KUINGIA KWENYE WEBSITE,KUDOWNLOAD BONYEZA HAPA
 
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: