Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta amesema  ndoto ya kutambulika katika medani ya soka duniani inatarajia kutimia muda mfupi ujao.


Nahodha huyo wa timu ya taifa, 'Taifa Stars' alisema hatua ya jina lake kuwemo katika orodha ya nyota 30 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mafanikio makubwa.

Majina mengine ya wanasoka wanaocheza Ulaya yaliyotajwa na Shirikisho la Soka Afrika (Caf) ni Mohamed Salah (Misri/Liverpool), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon/Borussia Dortmund) na Eric Bailly (Ivory Coast/Manchester United).

"Naanza kuona ndoto yangu inaanza kuwa kweli. Ni faraja jina langu kuwemo katika orodha ya washindani," alisema Samatta anayecheza soka ya kulipwa katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji.

Mchezaji huyo mwenye miaka 24, alisema kuwa hatua ya kutajwa kuwania tuzo hiyo ni fursa kwa wachezaji wa Tanzania kujifunza.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa TP Mazembe Englebert ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), alisema anatarajia kupata mafanikio Genk.

Samatta, alishindwa kuendelea na mchezo wa Jumamosi, baada ya kuumia katika mchezo waliotoka suluhu na Lokeren hatua iliyoibua hofu kama ataitumikia Taifa Stars dhidi ya Benin.

"Nasubiri taarifa ya daktari wa klabu yangu ndio nitajua kama nitajiunga na Taifa Stars kwa mchezo wetu na Benin au vinginevyo," alisema Samatta.

Taifa Stars inatarajia kujitupa uwanjani ugenini kumenyana na Benin katika mchezo uliopangwa kuchezwa Novemba 11.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: