ads

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Amissi Tambwe, amesema atarejea kwa kishindo kwenye kikosi cha timu hiyo baada ya kupona majeraha yake., amesema atarejea kwa kishindo kwenye kikosi cha timu hiyo baada ya kupona majeraha yake.


Tambwe hajaichezea timu hiyo msimu huu kutokana na kuwa majeruhi, kwa sasa na anaendelea kuimarika huku akitarajiwa kurejea uwanjani kwa wakati.

"Naumia sana kukaa nje, kazi yangu ni mpira hivyo ninapokuwa nje kwa sababu zozote naumia sana, ila nawaahidi mashabiki nitarejea uwanjani hivi karibuni na nitapambana kuhakikisha timu yetu inapata matokeo mazuri," alisema Tambwe.

Alisema kuwa bado kuna michezo mingi ya Ligi Kuu, hivyo timu yake inauwezo mkubwa wa Kufanya vizuri msimu huu.

"Kwangu naona Yanga haijafanya vibaya, kuna michezo mingi kwenye ligi hivyo bado nafasi ya kufanya vizuri na kutetea ubingwa wetu upo," alisema Tambwe.

Alisema kwa sasa amepona na anaendelea kuimarika na anategemea kujiunga na timu pindi itakaporejea Dar es Salaam kutoka Singida.

Yanga inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo Michezoni ya SportPesa, juzi ililazimishwa sare tasa na Singida United ambayo nayo inadhaminiwa na kampuni hiyo.

Kwa matokeo hayo, Yanga sasa ina pointi 17 sawa na Mtibwa Sugar.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: