
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamaganda Kabudi amesema majadiliano yanayofanywa na Serikali pamoja na Kampuni ya Dhahabu yaBarrick kuhusu mchanga wa dhahabu (makinikia) yamefikia mahali pazuri na kwamba Taifa litajulishwa hivi karibuni.
Kwa upande wa Tanzania timu ya majadiliano iliyoundwa na Rais John Magufuli ilikuwa iliongozwa na Profesa Kabudi wakati timu ya Barrick iliongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Richard William.
Kamati hiyo ambayo ilianza majadiliano hayo rasmi Julai 31 mwaka huu ilenga kujadiliana madai ya Tanzania kwenye biashara ya madini.
Akizungumza na wakuu wa taasisi, idara na vitengo vya sheria Serikalini mjini hapa, Kabudi alisema Taifa litataarifiwa kuhusu maendeleo ya majadiliano hayo hivi karibuni.
“Juzi na jana tumefikia katika hatua nzuri ambayo nisiseme lakini Taifa litataarifiwa hivi punde juu ya maendeleo ya utekelezaji wa tuliyokubaliana,”alisema.
“Baada ya hapo nilidhani nitapumzika nifanye kazi nyingine lakini mheshimiwa Rais amenipa jukumu jingine la kusimamia madini ya Tanzanite na Almasi.”
Alisema shughuli hizo ndizo zimemfanya iwe vigumu kuwatembelea na kuongea nao tangu alipochaguliwa kushika nafasi hiyo mwanzoni mwa mwaka huu.
Alisema miongoni mwa sababu ambayo iliwafanya wasiweke hadharani
wajumbe wa tume hiyo wanaoenda kukutana na kampuni ya Barrick kuepuka
watu kuwachambua kwa faida ya upande wa pili.
Alionya tabia ya wataalam wa sheria kutoa maoni ya kisheria haraka sio nzuri katika kushughulikia maslahi ya Taifa.
“Tutashindwa, tutalipa fedha nyingi wakati wake si huu. Tutalipa mabilioni ya fedha tukienda mahakamani. Kwa hiyo alipwe sio wakati wake. Na kwa unyenyekevu mkubwa tulipoanza majadiliano haya tuliambiwa kuwa Barrick watawashtaki,”alisema.
“Mtalipa fedha nyingi, wametushtaki? Nawaulinza nyinyi ndugu zangu wametushtaki Barrick? Tumelipa hela nyingi? Lakini sio ndio ilikuwa mazungumzo hayo? Kwamba hapo simesaini (Makubaliano). Subirini mtashtakiwa, mtalipa fedha nyingi.”
Alisema wengine walisema kuwa Barrick hawatafika katika mazungumzo hayo na kuhoji kama walikuja ama la.
“Mazungumzo yamevunjika. Sasa mlitaka tuyafanye hadharani? Moja ya sababu ya wale kufichwa isipokuwa mimi nifahamike wala ilikuwa hatuwaogopi sana wale. Nyinyi Watanzania maana mngeanza kuchambua huyu darasa la nne alifeli,”alisema.
“Kwa hiyo mngeanza kuchambua watu kwa faida ya yule (Barrick) badala ya kupeana. Hatukukutana na watu wadogo. Jana tulikuwa na Richard
Willison (Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick… komandoo yule (Willison) lakini pamoja na ukomandoo wake si tulipambana naye bwana?”
Alisema ni lazima kusimamia maslahi ya Serikali bila woga wowote na kwamba inakera kusikia mwanasheria akisema kesi ni ngumu nakwamba Serikali ilipe fedha haraka sana.
“Tutashtakiwa sasa wewe umeajiriwa kwasababu gani? Si uende upambane.
Nasema hili mjue nyakati zimebadilika. Mjiulize zimepitishwa sheria mnazifahamu zilizopitishwa si za wizara yako?”alihoji.
Pia alisema kuwa kwa muda wote wa majadiliano ya makinikia wajumbe wa timu hiyo hawakukaa majumbani kwao kutokana na uhalisiana wa suala hilo.
Post A Comment: