ads

Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Omar Mahita amesema baadhi ya askari polisi wanashindwa kuwachukulia hatua za kisheria viongozi wanaovunja sheria za nchi wakihofia kupoteza nafasi zao za kazi.


Akizungumza hayo wakati maadhimisho ya miaka 10 ya Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPFN), jana Novemba 8 amesema  askari wanatakiwa  kuwa na ujasiri.

“Askari wanatakiwa wakiwa kazini wasisite kumchukulia hatua   kiongozi yeyote watakayemkuta  na makosa’’amesema

Mahita amesema askari polisi wanakuwa waoga hawataki kuthubutu hivyo wanatakiwa kuwa jasiri hata kama lolote litatokea.

“Kwa nini askari wengi hawataki kuthubutu wanataka kulinda kazi zao hivyo wanatakiwa wapambane na wawe jasiri na wasipofanya hivyo ipo siku itawarudia,”amesema Mahita.

Naye Kamishna wa Polisi Jamii nchini,Musa Ali Musa ameutaka Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPFN) kufuata  maadili ya kazi na kuendelea kufanya  kazi kwa ujasiri  kwa mujibu wa sheria za nchi.

Musa amesema maadhimisho hayo  yataleta mafanikio kwa Jeshi la Polisi na nchi  kwa ujumla hivyo wataweza kufanya  tathimini ya  kutambua mafanikio na mapungufu yaliyojitokeza.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: