Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema hakuna waziri mwenye ubavu wa kukataa akimtuma jambo.


Amesema hayo jana Ijumaa Novemba 24,2017 katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Moita Bwawani akimnadi mgombea wa CCM wa Kata ya Moita wilaya ya Monduli, Prosper Damuni.

"CCM ndiyo chama kilichoshika dola kama kuna changamoto sehemu yoyote namwambia waziri anayehusika anafika haraka eneo hilo kusikiliza na kutatua changamoto hiyo, hakuna waziri mwenye ubavu wa kukataa nikimtuma," amesema Kinana.

Katibu mkuu huyo amewaomba wananchi katika kata 43 zinazofanya uchaguzi mdogo wa udiwani kuwachagua wagombea wa CCM akisema ndicho chama kinachoongoza dola na ahadi zinazotolewa zinatekelezeka.

Kinana amewaomba wananchi hao akisema ni wakati muafaka kwao kuacha kupiga kura kwa ushabiki.

Amesema wilaya hiyo inakusanya mapato ya ndani ya Sh2 bilioni kwa mwaka wakati bajeti yao kwa mwaka ni Sh49 bilioni kwa mwaka fedha ambazo zinatolewa na Serikali Kuu hivyo ni muhimu kuwa na diwani anayetoka chama hicho ili kurahisisha maendeleo ya wananchi.

Kinana amesema anafahamu wilaya hiyo ina changamoto mbalimbali ambazo zinahitaji kutatuliwa.

"Nataka nimpe mbinu mgombea wenu akichaguliwa anatakiwa kuwa karibu sana na mkurugenzi mtendaji wa wilaya na kwa kuwa anatokana na CCM atakuwa na uwezo wa kuingia na kutoka kwenye ofisi za Serikali kutafuta fedha za maji, barabara, afya na elimu hiyo ndiyo kazi ya diwani si kukaa tu kusubiri maendeleo yaje," alisema Kinana

 Katika mkutano huo uliohudhuriwa na wakuu wa mikoa, Mrisho Gambo wa Arusha na Christopher ole Sendeka wa Njombe waliwataka wananchi kutoyumbishwa na kelele za vyama vingine bali wamchague mgombea wa CCM.

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: