KIUNGO wa Simba, Ibrahim Mohammed 'Mo Ibrahim' amesema, habari za kwake kujiunga na Yanga ni stori tu, yeye hana hata mpango wa kwenda huko.


Mo Ibrahim ambaye hakuwa kwenye wakati mzuri ndani ya kikosi chake kutokana na kusumbuliwa na matatizo ya kifamilia.

Amesema, anasikia tetesi hizo  kama  watu wengine lakini kwa sababu yeye ndiyo muhusika, ameamua kutoa la moyoni na kusema, hakuna kitu kama hicho.

"Hakuna mpango huo, mimi ni mchezaji wa Simba achana na habari za Yanga. Sijui chochote na mimi nasikia tu kama wewe unavyosikia, watu wanapenda kuzungumza sana sijui kwa nini,"alisema Mo Ibrahim ambaye baada ya kuulizwa kama alishapigiwa simu na viongozi wa Yanga, Mo hakutaka kufunguka kwa undani akabaki amenyamaza tu.

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: