
Subscribe ndio neno gumu zaidi kwa wabongo kuliko kutafuna jiwe kama ilivyo kwa Waingereza kutamka Mwanjelwa..husema Monjela
Pamoja na vionjo hivyo..kwenye Simba Day ya mwaka huu ntakuja na style tofauti ya kutambulisha wachezaji...njoo ushuhudie mwenyew..usingoje kuhadithiwa ni Jtano hii pale dimba la Taifa... #SimbaDay #KibingwaZaidi 🇵🇪🇵🇪
Serikali yatoa tamko kuadimika mafuta ya kula nchini
Waziri Kigwangalla atetea ununuzi wa ndege
Zitto Kabwe amshauri Job Ndugai
Bunge lataka tende zifutwe kodi mfungo wa Ramadhani
Mo Dewji afunguka jinsi anavyopiga pesa kupitia kilimo
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amejivua uanachama wa CCM na nyadhifa zake zote, akisema haridhishwi na mwenendo wa siasa nchini.
Nyalandu, ambaye alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika Serikali ya Awamu ya Nne, aliiambia gazeti la Mwananchi Jumatatu mchana kuwa ameamua kujiondoa CCM na ameiomba “Chadema wafungue malango yao” ili aweze kuungana nao.
"Nimeamua kujiuzulu nafasi yangu ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017," alisema Nyalandu ambaye video ya uamuzi huo imesambaa mitandaoni.
"Hali kadhalika, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa.
"Aisha, nimechukua uamuzi huu kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya Watanzania."
Kwa uamuzi huo, Nyalandu, ambaye aliomba ridhaa ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi uliopita, amejivua ubunge na nafasi nyingine zote alizokuwa akishikilia ndani ya CCM, ikiwa ni pamoja na ujumbe wa Halmashauri Kuu.
Post A Comment: