ads

Msanii wa filamu wa kike bongo Wema Sepetu ambaye wengi humtaja kuwa msanii mwenye nyota ya kupendwa na mashabiki, amefunguka kuwa anasaka mtu atakaye toka naye usiku wa uzinduzi wa filamu yake.


Kwenye ukurasa wake wa Instagram Wema Sepetu amendika ujumbe wa kumtafuta mtu huyo atakayekuwa naye usiku huo, kwani akisema raha ya tukio kama hilo lazima uwe na mtu pembeni yako, kwani anatarajia kuvunja kabati kwa kupendeza, lakini haitakuwa na maana kama atakuwa peke yake.

" Bado siku 4 tu, nilisema kuna tatizo, kupendeza nitapendeza tena sana tu ila sasa sina date wa kwenda naye raha ya zulia jekundu uwe na mtu... nani atajitolea kuwa mtu wangu kwa usiku huo wa kukumbukwa!?", aliandika Wema Sepetu.

Mwisho wa wiki hii Wema Sepetu anatarajia kuzindua filamu yake mpya inayoitwa 'Road to heaven' aliyoigiza na wasanii wengine wakali wa filamu, akiwemo mshindi wa tuzo ya muigizaji bora wa kiume EATVAwards 2016, Gabo Zigamba, muigizaji wa kike Grace Mapunda na Petit Man.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: