Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simion Sirro amesema jeshi lake linazo taafira za kuokotwa kwa miili katika bahari ya hindi na miili hiyo ipo mikononi mwa jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi.
Akizungumza na ITV, IGP Sirro alisema miili hiyo ipo kwenye utambuzi kwa kuchukuliwa vinasaba ili kujua ni raia wa nchi gani, na kisha litatangaza kwa watu walipotelewa na ndugu zao kwenda kuangalia kama ni jamaa zao.
"Jeshi la Polisi tayari lishachukua hatua za awali za utambuzi kwa kuchuliwa vinasaba vya maiti hizo ili kufahamu ni raia wa wapi na tukishakamilisha zoezi hilo tutatangaza watu waliopotelewa na ndugu zao kuja kufanya utambuzi," alisema Sirro.
Amesema licha ya watu kudhani kwamba mauaji hayo yamefanywa na Polisi, jeshi hilo huwa halina kificho na kwamba kama ikitokea wakaua watu kwenye mapambano huweka wazi badala ya kwenda kuwatumbukiza baharini.



Post A Comment: