ads

MAMENEJA na wakurugenzi Tanesco walioshindwa kukamilisha agizo la Naibu Waziri wa Nishari na Madini la kuwaunganishia umeme watu waliokwishalipa fedha watashushwa vyeo.


Meneja wa Tanesco kanda ya Magharibi , mkoani Tabora, Maclean Mbonile, ameagizwa kuorodhesha majina ya wakurugenzi na mameneja, ambao hawakutekeleza maagizo ya Naibu Waziri Dk. Medard Kalemani ya kuwaunganishia umeme watu waliokwishalipia gharama ili watumbuliwe.

Akitoa maagtizo hayo Kalimani alisema kuwa viongozi hao wa Tanesco walipewa mwisho wa kufanya hivyo ifikapo Julai 31, wawe wamekwisha kuwaunganishia umeme watu katika maeneo yao.

Hata hivyo hadi sasa alipewa orodha ya wateja 14 pekee kuwa ndiyo walokuwa wamepewa huduma hiyo.

Naibu Waziri aliendelea kuzungumza kwenye utambulishaji wa mkandarasi na uzinduzi wa mradi wa kusambaza umeme wa vijijini (REA) awamu ya tatu katika kijiji cha Kisanga wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.

Alisema kuwa amewapa muda hadi ifikapo mwezi huu wawe wamemaliza kuunganisha umeme kwa watu hao na wakishindwa kufanya hivyo katika muda uliopagwa kama hawatokamilisha atawashusha vyeo.

Aliwaambia kuwa hataki kusikia kisingizio chochote cha kuhusu milingoti wala transfoma kwani vitu vyote vipo hapa nchini na wala si vya kuagiza nje.

Aidha Dk Kalemani alimtaka Meneja wa Tanesco Kanda ya Magharibi ajenge ofisi karibu na wananchi ili iwe rahisi kwao kupeleka malipo haraka pia ahakikishe wananchi wanapowawekea umeme wa rea waorodheshwe majina yao kwenye ofisi za Tanesco.

Kwa upande mwingine Naibu Waziri alisema kuwa katika maagizo aliyotoa hakuna ruhusa kwa mtaalamu yeyote wa Tanesco kufuatwa na mteja ofisini isipokuwa Tanesco ndiyo inapaswa kuwafuata wateja wao.

Hata hivyo alisema kuwa ole kwa mfanyakazi yeyote wa Tanesco atakayekutwa ofisini amekaa atakiona cha moto na kuondolewa kazini pasipo kuangalia huyu ana nafasi gani katika ofisi hiyo.

Maagizo hayo yazingatiwe alisema na kuongeza kuwa Tanesco ndiyo wasimamizi wa kuhakikisha wanawasimamia makandarasi na wafanye kazi usiku na mchana kuhakikisha wanamaliza kazi kwa muda uliopangwa na serikali.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: