Serikali yakanusha madai ya CHADEMA kuwa hakuna viwanda vipya vilivyojengwa katika awamu ya tano kwa kusema serikali imesajili viwanda 2,536.
Serikali imesema; "kuna viwanda ambavyo vilitii masharti kama TBL, TCC na viwanda vya saruji Mbeya, Tanga na Twiga", "viwanda ambavyo Serikali inakusudia kuvirejesha ni vile ambavyo vilikiuka mikataba"
"Lengo la Serikali siyo kuviendesha bali kuvitangaza kwa wawekezaji wenye uwezo wa kuviendesha"
"Katika awamu 5 jumla ya viwanda vilivyosajiliwa ni TIC-224, EPZA-41, BRELA-128 na SIDO-2,143". Takwimu za Julai 2016-Machi 2017 zinaonesha jumla ya biashara 7,277 zilifunguliwa na biashara mpya zaidi ya 224,738 zilisajiliwa
Hatua hii imekuja baada ya hapo jana CHADEMA kudai kwamba Sekta binafsi ndizo zinajenga Viwanda. Walidai Mikopo ya kujenga Viwanda kwa mwaka 2015 ikua inakuwa kufikia 32% walikuwa wanakopa, ila sasa hawajakopa chochote yaani 0% katika mwaka 2017. Hivi viwanda vinavyofunguliwa ni viwanda vilivyotafutia mikopo Serikali ya Kikwete, Serikali hii haijajenga kiwanda hata kimoja.
Mbowe alidai kwamba tatizo la hii Serikali ni kwamba mtu akiwa na cherehani za kushona nguo nne wanaita ni kiwanda. Haya ni masihara.
Mbowe alidai kwamba Sekta ya viwanda, hana uhakika kama Waziri wake kama anajua biashara yoyote au kama aliwahi kuuza japo hata mkaa.
Post A Comment: