ads

MBUNGE wa Moshi Mjini (Chadema), Jaffary Michael amesema kinachofanya kiongozi aonekane bora kuliko mwingine ni uadilifu, uaminifu, uthabiti na uimara katika kusimamia rasilimali ili ziwaletee wananchi maendeleo.


Pia ameeleza kuwa ubora wa viongozi wa kuchaguliwa hasa Madiwani, Wabunge na Rais utapimwa kwa jinsi walivyoweza kuhamasisha maendeleo kwenye maeneo yao ya uwakilishi.

Katika waraka wake alioutoa jana kwa umma akitaka wananchi waelewe dhana ya kuchagua wawakilishi hao, Jaffary alisema kama kuna kiongozi anayetoa fedha zake atakuwa anatimiza wajibu wa kijamii unaotaka kila mwenye nafuu asaidie maendeleo ya wenye uhitaji, ikiwa ni pamoja na kuchangia shughuli za maendeleo.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: