ads

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, ameliomba jeshi la polisi kukomesha matukio yalioibuka hivi karibuni ya utekaji wa watoto wenye umri wa miaka mitatu hadi sita ambao wanapotea katika mazingira tatanishi.


Mh. Lema amesema matukio hayo ni mabaya na kwamba yanaleta taharuki na huzuni kwa wazazi na walezi hivyo ni vyema polisi wakachukua hatua za haraka kuwabaini watu wanaotekeleza vitendo hivyo na kuvikomesha.

Mbunge huyo amesema watekaji hao mara baada ya kuwateka watoto wanadaiwa kutoa barua za madai ya fedha kwa kificho ili wawaachie watoto na kwamba, endapo madai yao hayatakelezwa hutishia kuwaua.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Olkerian, Daudi Safari, amesema wasiwasi umezikumba familia nyingi kufuatia matukio hayo hali iliyosababisha wazazi na walezi kushindwa kutekeleza majukumu yao mengine wakitumia muda mwingi kuwalinda watoto wao.

Mpaka sasa watoto wanaodaiwa kutekwa nyara ni Maurine David, Ikram Salim, Ayoub Fred Bakari Salim. Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kuzungumzia matukio hayo zimegonga mwamba
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: