Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani na Mjumbe wa Halmashauri Kuu CHADEMA, Frederick Sumaye amefunguka na kusema msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ameshindwa kupokea kadi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutokana na kuchelewa mahakamani.
Frederick Sumaye amesema kuwa leo ilikuwa imepangwa Wema Sepetu pamoja na wenzake kukabidhiwa kadi za Chama na msanii huyo kuongea ya moyoni kulichomfanya kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na CHADEMA lakini zoezio hilo limeshindwa kukamilika kutokana na kesi yake inayoendelea leo Mahakama ya Kisutu Dar es Salaam.
"Leo kulikuwa na mwenzetu Wema Sepetu alisema kuwa ana jambo la kuwaeleza lakini kubwa alikuwa anajiunga rasmi na CHADEMA hivyo mimi kazi yangu leo ilikuwa kuwapa hizo kadi halafu wangewasalimia na kusema kwanini ameamua kuhama kutoka huko walikokuwa na kujiunga rasmi na CHADEMA, sasa kwanini jambo hili limekuwa gumu mwenzetu Wema Sepetu leo ilikuwa ni siku ambayo anakwenda mahakamani na tuliongea na mawakili walisema mpaka saa tano kesi ingekuwa imeshasikilizwa na saa sita sisi tungeanza kazi yetu lakini haijawa hivyo" alisema Sumaye
Sumaye aliendelea kusema kuwa "Mpaka sasa hivi taarifa yuliyonayo ni kuwa wameingia kwenye chumba cha mahakama lakini kesi bado haijaanza kusikilizwa kwa hiyo tukaona tukiendelea kuwaweka hapa haitakuwa vyema kwani tulisema saa sita, tukasema saa saba hivyo tunaweza kuendelea kuongeza muda na jambo lisitokee sidhani kama itakuwa vizuri kwa hiyo mimi naomba niwaombe radhi kwani imekuwa nje ya uwezo wetu"
Leo tarehe 1/08/2017 kesi ya Wema Sepetu ilihairishwa asubuhi na kupangwa tena kuanzwa kusikilizwa saa sita na nusu mchana kutokana na Wakili wa Wema Sepetu kutokuwepo mahakamani.
Post A Comment: