ads

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Ndugu Abdulrahman Kinana amefunguka na kusema kuwa hakuna Rais duniani kote ambaye awewahi kuja Tanzania mara nyingi na mkoa wa Tanga kama Rais Museveni. 


Kinana amesema hayo jana katika sherehe za Uwekaji wa Jiwe la Msingi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta katika eneo la Chongoleani Tanga na kusema kuwa Museveni ni ndugu yetu na si rafiki wa Tanzania.

“Hakuna Rais aliyewahi kutembelea Tanzania mara nyingi kama Museveni, hakuna Rais aliyewahi kutembelea Tanga mara nyingi kama Museveni, alikuwa akitusihi sana kujenga reli hapa Tanga  ila leo naona anafuraha kwamba reli haikuwezekana lakini bomba la mafuta limeonekana, lakini nampongeza  sana Rais Magufuli kwa sera zao nzuri na vyama vyao kuwezesha bomba la mafuta” alisema Kinana 

Kinana aliendelea kusisitiza kuwa 

“Nimemsikia Museveni akisema Tanzania na Uganda ni nchi ndugu na si marafiki, naona Rais Magufuli na Museveni wote wanasema siasa ni uchumi na uchumi ni siasa” alisema Kinana 

Aidha Rais wa Uganda Museven amesema kuwa Watanzania ni ndugu zake kabisa ila wazungu wote kwake ndiyo marafiki 

“Mimi siwezi kusema Watanzania rafiki hapana ni ndugu zangu, mkinikubali nafurahi hata msiponikubali mimi nitabaki kuwa ndugu yenu, hao watu weupe (Wazungu)  ndiyo wabaki kuwa marafiki” alisisitiza Museveni
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: