Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amenunua ndege yenye thamani ya Sh2.64 bilioni kwa ajili ya kusambaza injili.
Kabla ya Askofu Gwajima kusema kiasi alichonunulia ndege hiyo aliweka picha kwenye mtandao wake wa Instagram akiwa mbele ya ndege hiyo akisema hivi karibuni ataileta Tanzania kwa ajili ya kusambaza injili kwenye ufalme wa Mungu.
Akizungumza na gazeti la Mwananchi jana jioni, Askofu Gwajima alisema aliijaribisha ndege hiyo juzi nchini Marekani kutoka uwanja mmoja kwenda mwingine.
Alisema taratibu za kimaandishi zikikamilika serikalini, ndege hiyo itakuwa nchini ndani ya wiki tatu.
“Heshima kwa Mungu wetu! Ni ya kwetu wote mdogo wangu, siku moja nikupeleke kwenda kuandika habari mahali,” Askofu Gwajima alimwambia mwandishi wa habari hii.
Post A Comment: