Ubalozi wa Zambia nchini Afrika Kusini, umekanusha uvumi ulioenea kwenye mitandao ya kijamii kwamba, Rais wa kwanza wa Zambia Dk. Kenneth Kaunda, amefariki dunia.
Afisa wa ubalozi huo, Bi. Naomi Nyawali, amesema taarifa hizo za mitandaoni si za kweli na kwamba, Mzee Kaunda anatarajiwa kuruhusiwa kutoka hospitali ya University Teaching ya jijini Lusaka .
Taarifa zilisambaa zikidai kifo cha kiongozi huyo wa zamani mapema jana asubuhi baada ya kulazwa siku ya Jumanne wiki hii baada ya kupata matatizo madogo ya afya yake.
Makamu wa Rais wa Zambia, Inonge Wina pamoja na Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Dk. Chitalu Chilufya walimtembelea Mzee Kaunda hospitalini ambako alikuwa akipata matibabu na kueleza kwamba, anaendelea vizuri.
Post A Comment: