ads

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsi, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amesema ugonjwa wa homa ya Ini umetajwa kuwa ugonjwa hatari zaidi na wenye kuuwa watu wengi polepole, huku takwimu zikiwa zinaonyesha una maambukizo makubwa mara 10 kuliko ya UKIMWI.


Mhe. Ummy amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza na wanahabari katika kilele cha maadhimisho ya siku ya homa ya Ini duniani yaliyofanyika jana.

"Nikiwa Waziri mwenye dhamana ninachotaka kuwaeleza Watanzania kwamba ugonjwa wa homa ya Ini umetajwa kuwa ugonjwa wa hatari na unaouwa watu wengi polepole. Kati ya watu 100, wanane wanaweza kuwa na maambukizi sugu ya ugonjwa huo na mbaya zaidi wanaweza wasiweze kuonyesha dalili za ugonjwa", amesema Ummy.

Pamoja na hayo, Waziri Ummy ameendelea kwa kusema "kwa mara ya kwanza ugonjwa huu unapewa kipaumbele unaostahili na kupitishwa na Shirika la Afya duniani katika mpango mkakati wa kwanza wa homa ya ini na kuanza kufanya kazi kuanzia mwaka 2016 mpaka 2021. Sisi serikali ya Tanzania tumekubali mkakati huu wa kwanza kwa maana tunataka kutokomeza kabisa ugonjwa huu", amesema Ummy.

Kwa upande mwingine, Ummy amesema kati ya watu laki mbili mwaka jana (2016) waliochangia damu, asilimia sita wamekutwa na maambukizi ya virusi vinavyosababisha homa ya Ini.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: