ads

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewaondolea hofu watumiaji wa mitandao ya simu, wanaotaka kutumia huduma ya laini moja kwa mitandao yote, kuwa hatawakosa huduma zinazotolewa na makampuni ya simu.


Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Tehama wa mamlaka, Nehemia Mwenisongole, alisema hayo Jijini Arusha jana wakati akizungumza na waandishi wa habari. Alisema huduma hiyo itakuwa ya hiari kwa watumiaji wa mitandao ya simu na itawasaidia kuondokana na kumiliki utitiri wa laini nyingi za simu na kutumia laini moja, iliyobeba mitandao yote ya simu ambayo atahitaji kutumia.

“Ukiamua kuhamia kwenye mfumo huu wa kuunganishwa kutumia namba moja, hakutakuwepo na madhara ya kuanza kuwaza kuwa wapo watu ambao nitawapoteza nikiingia huko,’’ alisema. Alisema kuingia kwenye mfumo huo, kutasaidia kuondoa changamoto ya kukosekana kwa mtandao mahali mtumiaji atakapokuwa na kumsaidia kutumia mtandao mwingine.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: