Kutokana na Katibu Mkuu wa Chama Dkt. Vincent Mashinji pamoja na viongozi wengine wa chama wakiwemo wabunge wawili, kuwekwa kizuizini kwa masaa 48 kinyume na Sheria za Nchi, ikiwa ni mwendelezo wa mamlaka za kiserikali kuvunja sheria na dalili za wazi za matumizi mabaya ya madaraka, Sekretarieti ya Chama Makao Makuu katika kikao kilichomalizika hivi punde, imeazimia yafuatayo;
1. Kuzitaka mamlaka zilizoagiza kukamatwa na kuwekwa kizuizini Katibu Mkuu Dkt. Mashinji pamoja na viongozi wengine hao 10 kinyume cha sheria za nchi, kuwaachilia huru mara moja kabla chama hakijachukua hatua zingine zinazotakiwa kulinda uhuru na haki za kikatiba na kisiasa zilizoko kwa mujibu wa sheria za nchi.
2. Iwapo itafikia kesho Jumatatu, tarehe 17 Julai, 2017 mamlaka hizo hazijamwachia huru Katibu Mkuu Dkt. Mashinji na viongozi hao 10 wanaoshikiliwa kizuizini kinyume cha sheria, Chama kupitia kwa Mwanasheria Mkuu wa Chama kitatangaza maamuzi yatakayochukuliwa kwenye mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika hiyo kesho.
3. Katika hatua ya sasa Sekretarieti pia imeelekeza kwa haraka Mawakili wa Chama kusimamia kesi dhidi ya Katibu Mkuu na Viongozi wengine kuhakikisha kuwa masuala ya kisheria yanafuatwa na haki kutendeka. Kwa sasa jambo hilo litasimamiwa na Wakili msomi Edson Mbogoro.
4. Aidha Sekretarieti imemteua Katibu ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Emanuel Masonga kukaimu kazi za Kanda ya Kusini wakati huu ambao Mwenyekiti na Katibu wa Kanda hiyo wakiwa kizuizini
Pamoja na Katibu Mkuu Dkt. Mashinji, viongozi wengine walioko kizuizini huko Mbambabay tangu jana walivyokamatwa hadi sasa ni kama ifuatavyo; 1. Mwenyekiti wa Kanda ya Kusini na Mbunge wa Jimbo la Ndanda Cecil Mwambe 2. Katibu wa Kanda Philbert Ngatunga 3. Ofisa wa Operesheni na Mafunzo Manawa Samuda 4. Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma Zubeda Sakuru, 5. Ofisa wa Kanda ya Kusini Asia Mohamed 7. Mwenyekiti wa Mkoa wa Ruvuma Ireneus Ngwatura 8. Katibu wa Mkoa wa Ruvuma Delphin Ngaiza. 9. Mwenyekiti wa Wilaya ya Nyasa Cuthbert Ngwata, 10. Katibu Mwenezi wa Wilaya ya Nyasa Charles Makunguru.
*Tumaini Makene*
*Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasilian
Post A Comment: