ads

Rais John Magufuli, amemtumia rambirambi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kutokana na kifo cha mkewe  Linah kilichotokea usiku wa Julai 15.


Linah amefariki dunia katika Hospitali ya Aga Khan, jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa ya Ikulu imesema, Rais Magufuli ameeleza kushtushwa na kusikitishwa na kifo hicho.

Amsema pamoja na familia yake wanaungana na Dk Mwakyembe katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

“Nakupa pole sana Dk Mwakyembe kwa kuondokewa na mkeo mpendwa Linah, natambua hisia za maumivu ulizonazo wewe na familia nzima, nyote nawaombea Mwenyezi Mungu awatie nguvu, awape subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi,” amesema Rais Maguful
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: