KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi amefunguka kwa sasa anaendelea na mazoezi na kikosi hicho ambapo mashabiki ambao wana hofu na uwezo wake wamsubiri uwanjani kwenye mechi dhidi ya Rayon Sport ya Rwanda, kwenye mechi ya Simba Day.
Mganda huyo amefanikiwa kurejea kwa mara nyingine ndani ya Simba kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Villa ya Uganda ambapo kwa sasa yupo nchini Afrika Kusini kwenye kambi ya timu hiyo chini ya kocha wake, Joseph Omog raia wa Cameroon.
Akizungumza na gazeti la Championi Jumatatu, Okwi mmoja wa wachezaji waliokuwepo kwenye ubingwa wa mwisho wa Simba, amesema anaendelea na mazoezi na wenzake kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Simba Day dhidi ya Rayon ambao ndiyo utakuwa wa kwanza ndani ya kikosi hicho tangu kurejea kwake.
“Tunaendelea na mazoezi ya pamoja ya kujiandaa na msimu ujao, lakini kwa wale ambao wana hofu juu ya nini nitakachokifanya basi niwaambie kuwa nitawaonyesha makali yangu kwenye mechi ya Simba Day ambayo itakuwa ya kwanza kwetu nchini Tanzania,” alisema Okwi aliyewahi kucheza soka la kulipwa Denmark.
Post A Comment: