ads

Kamati Kuu ya CHADEMA   imekutana kwa siku mbili, tarehe 29-30 Julai, 2017 katika Hotel ya Double Tree, jijini Dar es Salaam kujadili hali ya siasa nchini pamoja na ukandamizwaji wa demokrasia .


Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje, John Mrema inasema kwamba katika mambo ambayo Kamati Kuu imejadili ni pamoja na kamata kamata inayoendelea kufanywa na vyombo vya dola dhidi ya viongozi, wanachama na wafuasi wa CHADEMA maeneo mbalimbali nchi nzima. 

Hata hivyo kikao hicho kimejadili na kufikia maadhimio na hatua za kuchukua katika ajenda ni pamoja na  kuporomoka kwa uchumi na hali ngumu ya maisha kwa watanzania, ambapo  taarifa kamili juu ya maadhimio hayo na hatua zitakazochukuliwa na chama itatolewa leoJumatatu tarehe 31 Julai 2017, kwenye kikao na waandishi wa habari kitakachofanyika jijini Dar es salaam.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: