ads

MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Nchini (TCAA), inatarajiwa kununua rada nne kwa ajili ya kumulika anga la Tanzania mpaka nje ya nchi.


Kwa mujibu wa Mwanasheria Mwandamizi wa TCAA, Maria Memba, rada iliyonunuliwa hivi karibuni ni ya mwaka 2002. Alisema ili kukamilisha ununuaji wa rada hizo, TCAA ipo katika hatua za kukamilisha mkopo, utakaowawezesha kununua rada hizo kwa gharama za Euro milioni 22 (Sh bilioni 43).

“Rada hizi zitafungwa Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Uwanja wa Kimataifa wa Songwe (SIA) na Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Alisema mkopo huo utakapopatikana, mradi huo unatarajiwa kuchukua miezi 18 tangu kusainiwa kwa mkataba. “Mradi huo ni sehemu ya mkakati wa TCAA kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za uongozaji ndege ili kutoa huduma hizo kwa haraka, tija na kuongeza usalama katika sekta ya usafiri wa anga nchini na duniani,” alisema.

Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, Hamza Johari alinukuliwa akisema mradi huo ukikamilika utakuwa na faida nyingi kiusalama, kwani kwa kutumia rada mwongoza ndege anaweza kuongoza ndege nyingi zaidi kwa ufanisi na kuongeza mapato.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: