ads

Baada ya kukamilisha uhamisho wa kujiunga na klabu ya  Difaa Al Jadida ya Morocco, mshambuliaji Simon Msuva amesema nchi hiyo ni njia ya kuelekea barani Ulaya.


Mshambuliaji huyo alisaini mkatana wa miaka mitatu wa kuichezea Jadida, mkataba ambao unahitimisha miaka mitano ya kuichezea Yanga aliyojiunga nayo 2012 akitokea Moro United ya Morogoro.

Mwananchi kupitia vyanzo vyake mbalimbali, linafahamu kuwa Msuva amesajiliwa kwa dau la zaidi ya 200 milioni za Tanzania.

Akizungumza na MCL Digital baada ya kusaini mkataba huo, mchezaji huyo alisema hiyo ni fursa kubwa kwenye maisha yake ya soka.

“Mimi ni mchezaji ninayejiamini na hata kufika hapa ni kutokana na kupambana, ninaamini milango zaidi itafunguka kutoka hapa, nimeanza maisha mapya. Jukumu langu ni kufanya kazi kwa bidii,” alisema Msuva.

Hata hivyo mfungaji huyo bora wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2018/17 alisema haitakuwa kazi rahisi kwake kupata nafasi ya kuanza kikosini.

“Itakuwa ngumu kupata nafasi, lakini niko tayari kwa changamoto hiyo. Mimi ni mchezaji ninayejiamini,”alisema Msuva aliyeibukia kisoka katika klabu ya Azam.

Credit - Mwananchi
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: