ads

Mbunge wa Jimbo la Geita Vijijini, Joseph Msukuma, ameongoza wapiga kura wake wa kijiji cha Hiyanamilo, Kata ya Nkome Wilayani Geita, kutoa visiki ambavyo viliwekwa na mtu ambaye nasadikika amenunua eneo la kijiji linalokadiliwa kuwa ni hekari moja na nusu ambalo lilitengwa kwa matumizi ya stendi.


Hatua hiyo imekuja baada ya Serikali ya Kijiji ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Thomas Alila na Mtendaji wa kijiji, Charles Mbilingi, kuuza eneo kwa kiasi cha shilingi Milioni sita (6).

Kwa mujibu wa Mbilingi, tarehe 15 mwezi huu walikaa kwenye kikao na wanakijiji na kuamua kwamba wauze eneo hilo ili lisaidie ujenzi wa shule.

Hata Hivyo, kutokana na maelezo hayo ya Mtendaji wa Kijiji, Msukuma aliwaeleza wananchi ambao walikuwa kwenye mkutano wa hadhara kuwa eneo hilo liliuzwa tarehe tano mwezi huu jambo ambalo yeye alilikataa kutokana na faida ambazo zinaweza kupatikana kutokana na uwapo wa eneo hilo.

"Nimesikitishwa sana na kitendo ambacho kimefanyika cha kuuzwa eneo hilo kiasi cha Sh. milioni 6 na mimi nilimpigia simu mtendaji, nikamwambia azirudishe pesa, aende halmashauri kuna maelekezo kwa mkurugenzi na tutambue kuna maeneo muhimu lazima yawepo. Leo ninakwenda kung'oa visiki vyote," alisema Msukuma.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: