Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amesema anataka kuiongoza Manchester United kwa miaka 15 zaidi ili kuirejesha furaha kwa mashabiki wa klabu hiyo kama enzi za Sir Alex Ferguson.
Kocha huyo maarufu ‘Special One’ tangu aingie Manchester United msimu uliopita, amemaliza kwa mafanikio makubwa baada ya kutwaa Kombe la Capital One na Europa huku akiamini msimu wake huu wa pili atafanya makubwa zaidi.
Hivyo, Mourinho anaamini iwapo atakaa klabuni hapo kwa miaka 15 ataifanya Manchester United kuwa kama ya kipindi cha Ferguson.
Post A Comment: