Mahakama ya Kisutu imeamuru mmiliki wa Kampuni ya IPTL, Harbinder Seth apewe matibabu kutokana na matatizo ya kiafya yanayomkabili huku ikiahirisha kesi inayomkabili yeye na mfanya biashara James Rugemalila na kuwataka kurejea mahakamani Agosti 3.
Kesi hiyo imeahirishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya wakili wa serikali kueleza kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.
Harbinder Seth pamoja na James Rugemalila wanakabiliwa na na mashtaka 12, yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababisha serikali hasara.
Post A Comment: