Rais John Magufuli jana ametoa siku 14 kwa wamiliki wa vituo vya vyote mafuta nchini, kuhakikisha wanaweka na kutumia mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFDs) na atakayekiuka agizo hilo atafutiwa leseni ya biashara yake.
Rais Magufuli ametoa agizo hilo wakati wa ufunguzi wa barabara ya Kigoma-Biharamulo-Lusahunga yenye urefu wa KM 154 huku akiwataka mawaziri wenye dhamana kuhakikisha wanafuatilia maagizo hayo kuanzia sasa.
"Wanaolalamika kukosa mafuta waendelee kufanya hivyo, ni mara mia tukose mafuta kuliko kuwa na wafanyabiashara wanaokwepa kodi", amesema Rais Magufuli.
Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amepiga marufuku wananchi kutozwa kodi kwa mzigo wenye uzito wa tani moja anapousafirisha kutoka wilaya moja kwenda nyingine.
Post A Comment: