ads

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema),  Tundu  Lissu amekamatwa jana, Alhamisi, Julai 20 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA)  akielekea Kigali, Rwanda  kwenye kikao cha Halmashauri ya EALS kinachoanza leo.


Kamanda wa polisi viwanja vya ndege, Martn Ortieno amesema kwamba ni kweli wamemkamata Lissu ambaye pia ni Mwanasheria wa Chadema na kwamba amepelekwa makao makuu ya Polisi.

Hata hivyo, kamanda huyo hakutaja sababu za kukamatwa kwa mwanasheria huyo.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema,  John Mrema amesema kwamba mwanasheria huyo amekamatwa  jioni hii.

Mrema amesema Lissu amekamatwa na watu waliojitambulisha kwamba ni maofisa wa polisi kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam.
ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: