Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Mhe Amina Mohammed amewasilisha Ujumbe Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya, Mhe Uhuru Kenyata kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga.
Ujumbe huo kutoka kwa Rais Kenyatta unakuja kwa Rais wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli ambapo ulipokewa na Dk.Augustine Mahiga jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli.
Katika mazunguzmo yao, Mawaziri hao wamekubali kwa pamoja pendekezo la kuunda Kamati itakayoongozwa na wao wenyewe ambayo itakuwa na jukumu la kutafuta suluhu ya haraka inapotokea migogoro ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili.
Credit - Habari Leo
Post A Comment: