Rais John Magufuli ametoa Sh1milioni kwa ajili ya kutengeneza dirisha la bweni alilolivunja wakati akiwa kidato cha pili pamoja na madirisha mengine yanayohitaji matengenezo.
Rais Magufuli amesomea elimu ya sekondari katika Seminari ya Mtakatifu Karoli Lwanga ambapo ameendesha harambee iliyofanikisha kupatikana mifuko 1,000 ya saruji na mabati 150 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa majengo ya seminari hiyo.
Akiwa njiani kuelekea Ngara, Rais Magufuli amesimamishwa na wananchi wa Nyakahura na akawahakikishia kuwa Serikali itaifanyia matengenezo Barabara ya Nyakahura–Rusumo–Ngara.
Pia ameahidi kumtuma Waziri wa Maji na Umwagiliaji kwenda kuangalia namna ya kutatua tatizo la maji na pia amechangia Sh 10 Milioni katika ujenzi wa majengo ya shule.
Kesho Julai 20, 2017 Rais Magufuli ataendelea na ziara yake Mkoani Kagera ambapo hapa Ngara atazungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara utakaofanyika mchana.
Post A Comment: