ads

Zoezi la utafutaji, ufuatiliaji na ukaguzi wa wadaiwa sugu na ambao wamenufaika na mikopo ya elimu ya juu mahala pa kazi iliyoendeshwa na Bodi ya Mikopo ya Mikopo ya Elimu ya Juu katika kipindi cha mwaka mmoja, limefanikiwa kwa asilimia 46 na kupelekea makusanyo ya mikopo hiyo kuvuka lengo lililokusudiwa.


Akiongea na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, kuhusiana na hali ya makusanyo ya mikopo kwa wanufaika wa elimu ya juu, Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Bwana Abdulrazak Badru amesema walilenga kukusanya Shilingi Bilioni 76 lakini wamekusanya Shilingi Bilioni 116 ikiwa ni kiwango cha marejesho cha asilimia 46.

Bwana Badru amesema, hataacha kutumia mbinu ya ufuatiliaji mahala pa kazi huku akiwakumbusha wale ambao wanashindwa kurejesha mikopo kwa hiari sheria itafuata mkondo dhidi yao kwani fedha hizo hutumika kwa wanafunzi wa awamu mpya ya masomo.

Aidha, Bwana Badru ametoa onyo kali kwa waajiri ambao wameshindwa kuwasilisha majina ya waajiriwa wao ndani ya siku 28 kwa bodi hiyo, kuchelewesha makato baada ya kuwakata waajiriwa ama kuficha taarifa kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

ads
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya SWAHILI NEWS kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
Share To:

SWAHIBA MEDIA STAFF

Habari , karibu katika mtandao wetu ili kuhabarika na stori zote za siku katika lugha yetu adhwim ya kiswahili, habarika wakati wote weka dunia kiganjani mwako na swahili news

Post A Comment: